Loading...

Jiji la Dar namba 6 kwa maambukizi ya VVU katika bara la Afrika.

Licha ya jitihada za Serikali na wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi, hali katika Jiji la Dar es Salaam si shwari baada ya kushika nafasi ya sita barani Afrika kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Dar es Salaam inashika nafasi hiyo kwa kuwa na watu 210,000 wanaoishi na virusi vya Ukimwi, kati yao asilimia 58 ni wanawake.


Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya Ukimwi duniani kutoka Shirika la Mpango wa Ukimwi la Umoja wa Mataifa (UnAids) kwa mwaka 2015, Jiji la Dar es Salaam limeshika nafasi ya sita katika majiji barani Afrika yenye kiwango cha juu cha maambukizi ya Ukimwi.

Ofisa wa UnAids Tanzania, Fredrick Macha alisema asilimia 16 ya maambukizi mapya Tanzania Bara, yanatokea katika Jiji la Dar es Salaam.

ZeroDegree.
Jiji la Dar namba 6 kwa maambukizi ya VVU katika bara la Afrika. Jiji la Dar namba 6 kwa maambukizi ya VVU katika bara la Afrika. Reviewed by Zero Degree on 12/06/2016 10:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.