Loading...

Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] kukutana Jumamosi.

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) itafanya kikao chake cha kawaida Jumamosi ijayo.

Taarifa iliyotolewa jana na CCM ilieleza kuwa kikao hicho kitakuwa cha siku mbili na kitafuatiwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambacho kitafanyika Jumatatu ijayo.

“Vikao vyote hivyo vitafanyika jijini Dar es Salaam,” alisema taarifa hiyo iliyosainiwa na Selemani Mwenda kwa niaba ya msemaji wa chama hicho.

Pamoja na kutofafanua kwa undani ajenda za vikao hivyo, hata hivyo wachambuzi wa mambo ndani ya chama hicho wanaamini kuwa moja ya ajenda za vikao hivyo itakuwa ni uteuzi wa mgombea ubunge wa Jimbo la Dimani, Zanzibar.

Jimbo hilo kwa sasa halina mbunge baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wake, Hafidh Ali Tahir kufariki dunia hivi karibuni wakati akihudhuria vikao vya Bunge mjini Dodoma.

Pia kikao hicho kama ilivyo kawaida kitajadili hali ya siasa nchini tangu Rais Magufuli aingie madarakani mwaka mmoja uliopita.

Kwa sasa, Rais Magufuli amepiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa jambo ambalo limeleta malalamiko kutoka kwa wanasiasa wa mrengo wa upinzani.

Viongozi wa dini wamekuwa wanafanya jitihada kuzungumza na rais ili aweze kulegeza msimamo huo baada ya kukisihi Chama cha Demokrasia na Maendeleo kusitisha kampeni yake ya Ukuta ambayo ilikuwa ifanyike nchi nzima.

ZeroDegree.
Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] kukutana Jumamosi. Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi [ CCM ] kukutana Jumamosi. Reviewed by Zero Degree on 12/06/2016 10:07:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.