Loading...

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ahofia kupangwa na Klabu ya Juventus katika hatua ya mtoano.

Zidane amekiri hataki kukutana na Juventus kwenye hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kikosi hicho cha Zidane kilitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Borussia Dortmund juzi Jumatano na kumaliza hatua ya makundi wakiwa nafasi ya pili.

Hivyo Madrid wanaweza wakakutana na Arsenal, Napoli, Monaco au Leicester City kwenye droo ya robo fainali ya michuano hiyo itakayochezeshwa Jumatatu ya wiki ijayo, lakini Zidane amesema wakipangwa na timu yake ya zamani, Juventus itakuwa ratiba mbaya sana.

“Sijafikiria kuhusu droo, nilitaka tumalize vinara wa kundi na tulifanya kila kitu, lakini haikuwa hivyo,” alisema Zidane.

“Tutaona itakavyokuwa Jumatatu. Sitaki tukutane na Juventus, lakini hakuna jinsi na hatuwezi kuzuia hilo kutokea.”

ZeroDegree.
Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ahofia kupangwa na Klabu ya Juventus katika hatua ya mtoano. Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane ahofia kupangwa na Klabu ya Juventus katika hatua ya mtoano. Reviewed by Zero Degree on 12/09/2016 04:24:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.