Loading...

Liverpool wanatarajiwa kumruhusu Kiungo Lucas Leiva kutimkia Italy.

Pamoja kazi yake kuerekea mwishoni Anfield, Liverpool wanatarajiwa kumruhusu mchezaji wake wa muda mmrefu aondoke.

Kwa mujibu wa ESPN FC , Liverpool wako tayari kumuachia huru kiungo Lucas Leiva, ambaye kwa sasa anaitupia macho Inter Milan ya Siria A. Klabu hiyo ya Italia inasemekana iko tayari kuomuongeza Mbrazil huyo katika kikosini siku za usoni, na inaweza kufanya hivyo ama kwa mkopo au uhamisho wa kudumu.

Leiva, 29, alijiunga na Liverpool mwaka 2007 baada ya kuingia Ligi Kuu akitokea Brazil katika klabu ya Gremio na imeshiriki katika mechi zaidi 230 katika mashindano yote ambayo Liverpool imeshiriki.

Pamoja na kurejea kwa beki kijana, Joe Gomez katika mfumo wa Jurgen Klopp, klabu imeripoti kuwa ni rahisi zaidi kumruhusu Leiva kuondoka Anfield. Leiva ameonekana katika michezo 8 tu ya Ligi Kuu ya Uingereza na alikuwa akilazimika kucheza kama mbadala wa kwa Klopp ikiwa ni kuziba nafasi ya Gomez aliyekuwa majeruhi.

Liverpool kwa sasa inashikilia nafasi ya 3 katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza huku wakielekea kukipiga na Stoke City siku 
ya Jumanne, wakati huo wakiwa na tofauti pointi 9 kati yao na viongozi wa ligi Chelsea.

ZeroDegree.
Liverpool wanatarajiwa kumruhusu Kiungo Lucas Leiva kutimkia Italy. Liverpool wanatarajiwa kumruhusu Kiungo Lucas Leiva kutimkia Italy. Reviewed by Zero Degree on 12/27/2016 06:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.