Loading...

Mali za Chama Cha Mapinduzi [CCM] kumpeleka Kinana mkoa kwa mkoa.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jengo la kitega uchumi la chama hicho lililopo Upanga jijini Dar es Salaam jana.
Siku chache baada ya Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli kutaka mali za chama zihakikiwe, katibu mkuu wake, Abdulrahman Kinana ametangaza kuanza ziara za mkoa kwa mkoa kuzikagua.

Kabla ya ziara hiyo itakayoanzia Dar es Salaam, Kinana ametoa mwezi mmoja kwa viongozi wa mikoa kufanya uhakiki wa mali hizo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa jengo la ghorofa saba la CCM, tawi la Kibasila, wilayani Ilala lililogharimu zaidi ya Sh7 bilioni, Kinana alisema, “Tathmini yetu inaonyesha Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na mali nyingi, sasa nawapa mwezi mmoja mjiridhishe kabla sijaanza ziara yangu nitakayopita kila wilaya kukutana na wajumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya mkoa, mjiandae,” alisema.

Alisema kwenye ziara hiyo, yeye ndiye atakayeamua mali za kutembelea kwa sababu anazijua na kwamba, alishaagiza mikoa yote kuziorodhesha na kuwasilisha makao makuu.

Credits: Mwananchi
ZeroDegree.
Mali za Chama Cha Mapinduzi [CCM] kumpeleka Kinana mkoa kwa mkoa. Mali za Chama Cha Mapinduzi [CCM] kumpeleka Kinana mkoa kwa mkoa. Reviewed by Zero Degree on 12/16/2016 10:04:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.