Loading...

Mghana, James Katei anzaa mazoezi rasmi Msimbazi.

YULE mido Mghana, James Katei aliyetua nchini kwa ajili ya kuitumikia Simba, ameanza kazi yake rasmi kwenye mazoezi ya timu hiyo kwa kufanya vitu adimu uwanjani.

Simba inayojifua vilivyo kwenye Uwanja wa Kanisa la Bapstist mjini hapa kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara, imeonekana kutotaka masihara hata kidogo kwenye mzunguko wa pili.

Mido huyo namba sita pamoja na kwamba bado hajawa na uhakika wa kujumuishwa kikosini, lakini kazi yake imewagusa wengi na shughuli yake ni pevu uwanjani.

Wekundu hao wa Msimbazi walifanya mazoezi kutwa mara mbili baada ya kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog, kusikia watani wao wa jadi Yanga, wamekuwa wakijifua juani kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Yanga wanaoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 33 nyuma ya Simba wenye pointi 35, wamekuwa wakifanya mazoezi kuanzia saa nane mchana kwenye Uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam, chini ya kocha mkuu wao, George Lwandamina.

Wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakifanya mazoezi asubuhi na jioni na Simba wataanza kucheza na Ndanda Desemba 17, mwaka huu kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Katika mazoezi jana, Simba walianza kufanya mazoezi ya viungo na stamina kuhakikisha wanarejea makali yao ya mwanzo ambayo walicheza mechi 13 bila kufungwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Omog alisema mara nyingi wachezaji wanapokuwa likizo wanajisahau hivyo kupoteza ufiti wao, kwa hali hiyo amewaangalia kuhakikisha anawarejesha katika ufiti wao.

“Nina imani kubwa na vijana wangu, baada ya kuwapa mapumziko sasa tumerejea kazini, hivyo ninatarajia kucheza mechi za kirafiki kujiweka katika hali nzuri,” alisema Omog.

Omog alisema anahitaji kuona kikosi chake kinacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kwa lengo la kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili.

Alisema baada ya kuwepo kwa wachezaji wapya akiwamo kipa Danniel Agyei, anahitaji kuwa makini katika suala la mechi za kirafiki kuona uwezo wa wachezaji hao wapya.

“Nawapa mazoezi ya kuongeza stamina ili wachezaji wangu wamudu kucheza mpira, kwani nina imani mzunguko wa pili utakuwa wa ushindani mkali,” alisema Omog.

Simba itashuka dimbani leo kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Polisi Morogoro ili kuangalia ubora na upungufu wa kikosi chake na baadaye aweze kufanyia kazi.

Wachezaji waliokuwa Morogoro ni Vincent Angban, Peter Manyika, Daniel Agyei na Dennis Richard, Hamad Juma, Janvier Bokungu, Abdi Banda, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novaty Lufunga na Method Mwanjali.

Wengine ni Awadh Juma, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Said Ndemla, Mussa Ndusha, Muzamil Yassin, Jamal Mnyate, Shizza Kichuya, Frederick Blagnon, Laudit Mavugo, Ame Ally, Ibrahim Hajib, Malika Ndeule, Emmanuel Semwanza, Hajji Ugando na kiungo mpya, Mghana James Katei aliyewasili jijini juzi kwa ajili ya majaribio.

ZeroDegree.
Mghana, James Katei anzaa mazoezi rasmi Msimbazi. Mghana, James Katei anzaa mazoezi rasmi Msimbazi. Reviewed by Zero Degree on 12/09/2016 09:58:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.