Loading...

Mgombea kiti cha umeya Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi [CCM] apita bila kupingwa.

MGOMBEA wa umeya wa Mji wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Khatib Abrahman Khatib amefanikiwa kutetea nafasi yake baada ya vyama vyingine ya siasa kushindwa kuwasilisha majina ya wagombea kuwania nafasi hiyo.

Khatib aliibuka mshindi katika mchakato wa ndani ya CCM kwa kuibuka na ushindi wa kura 27 za wapiga kura wote, huku naibu meya akichaguliwa Bimkubwa Said Sukwa aliyepata kura 15 na kumshinda mpinzani wake Saleh Fasihi aliyepata kura 12.

Ofisa mmoja wa Manispaa ya Zanzibar ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake anayeshughulikia uchaguzi wa madiwani alisema hakuna majina ya wagombea wa vyama vingine yaliyowasilishwa kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa mwongozi wa uchaguzi huo, wajumbe wa baraza la madiwani watapiga kura kumchagua meya mpya kwa kuwajumuisha wagombea wengine wa vyama vya siasa ambao hadi sasa hawajawasilisha majina yao.

Akizungumza baada ya uchaguzi wa ndani ya CCM uliomteua Khatib, Naibu Katibu Mkuu wa CCM – Zanzibar, Vuai Ali Vuai aliwataka madiwani kufanya kazi kwa ajili ya kutekeleza na kusimamia ilani ya chama hicho tawala.

Alisema madiwani wanayo nafasi kubwa ya kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM kwa kuwaletea wananchi maendeleo ili kukabiliana na umasikini.

Alitoa mfano kuwa, madiwani wanawajibika kufanya kazi za kuleta maendeleo kama ilivyo kwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge katika majimbo ya uchaguzi. Vuai aliwapongeza watendaji hao katika majimbo ya uchaguzi kwa juhudi zao katika kutekeleza ilani ya uchaguzi pamoja na ahadi za viongozi hao katika majimbo ya uchaguzi.

ZeroDegree.
Mgombea kiti cha umeya Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi [CCM] apita bila kupingwa. Mgombea kiti cha umeya Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi [CCM] apita bila kupingwa. Reviewed by Zero Degree on 12/30/2016 03:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.