Loading...

Mwamba wa mawe wadondoka Mgodini, 5 wafariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya.

Watu watano wamefariki dunia na sita kujeruhiwa vibaya baada ya kudondokewa na mwamba wa mawe katika shimo la mgodi wa zamani wa Resolute, Nzega mkoani Tabora.

Mkuu wa wilaya ya Nzega, Godfrey Ngupulla alisema tukio hilo limetokea jana saa 7:00 baada ya kundi la wachimbaji wadogo wa mgodi wa Umoja kuvamia eneo hilo ambalo limepigwa marufuku na Serikali.

Alisema eneo hilo limezuiwa kuchimbwa kutokana na hatari iliyopo lakini baadhi ya wachimbaji wamekuwa wakiingia kwa kificho kuchimba.

Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Joseph Mpenda, mkazi wa shinyanga, Mohamed Mohamed mkazi wa Singida , Manona Nyombi mkazi wa Bariadi na Modesta Leonard mkazi wa Nzega.

Waliojeruhiwa ni Kangwa Mayenga mkazi wa Bariadi, Agness Antony mkazi wa Chato, Deus Alphonce mkazi wa Igunga na aliyefahamika kwa jina moja la Mapunda mkazi wa Chato.

ZeroDegree.
Mwamba wa mawe wadondoka Mgodini, 5 wafariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya. Mwamba wa mawe wadondoka Mgodini, 5 wafariki dunia na wengine kujeruhiwa vibaya. Reviewed by Zero Degree on 12/30/2016 05:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.