Loading...

Uongozi wa timu ya Azam umemtangaza Iddi Nassor kuwa kocha mpya.

Iddi Nassor akitoa maelekezo.
SIKU moja baada ya Azam kuachana na kocha wake raia wa Hispania Zeben Hernandez, uongozi wa timu hiyo umemtangaza Iddi Nassor 'Cheche' kuiongoza timu hiyo.

Kabla ya uteuzi huo, Cheche alikuwa kocha wa vijana wa timu hiyo na kwa sasa atasaidiana na Iddi Aboubakar kuiongoza Azam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Saad Kawemba alisema kwamba wamefikia makubaliano na makocha hao kutoka Hispania kuvunja mikataba yao.

Jopo hilo la makocha linaundwa na Kocha Mkuu Hernandez, Msaidizi wake, Yeray Romero, Kocha wa Makipa Jose Garcia, Kocha wa Viungo, Pablo Borges na Mtaalamu wa tiba za Viungo, Sergio Perez.

Kawemba amesema kwamba uamuzi huo umefikiwa na Bodi ya Wakurugenzi wa timu hiyo jana, na umetokana na mwenendo mbaya wa Azam FC kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambayo imefikia raundi ya pili hivi sasa.

"Azam FC inawatakia kila la kheri na mafanikio mema makocha hao huko waendako na inawashukuru kwa mchango wao wote walioutoa kwenye timu kwa kipindi chote walichokaa, ikiwemo kuwapa taji la kwanza la Ngao ya Jamii mwaka huu kwa kuifunga Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-1 kufuatia sare ya mabao 2-2,"alisema Kawemba.

Amesema wakati uongozi ukiwa katika mchakato wa kusaka kocha mpya, kikosi hicho kitakuwa chini ya Cheche Aboubakar ambaye ni kocha wa makipa.

Makocha hao walianza kazi juzi kukiandaa kikosi chao kw ajili ya michuano ya kombe la Mapinduzi itakayoanza Januari
"Azam FC inapenda kuwaambia mashabiki wake kuwa wawe watulivu katika kipindi hiki kwani uongozi umefanya uamuzi sahihi kwa ajili ya kuinyanyua timu juu ili hatimaye ushiriki wetu wa michuano mbalimbali uweze kuwa ni wa kiwango cha juu tofauti na hali ilivyokuwa sasa," alisema Kawemba.

Hernandez anaondoka Azam FC akiwa ameiongoza timu hiyo kwenye mechi 18 rasmi ambazo ni za mashindano, 17 za ligi na moja ya Ngao ya Jamii, amefanikiwa kushinda mechi nane, sare sita na kufungwa mara nne.

ZeroDegree.
Uongozi wa timu ya Azam umemtangaza Iddi Nassor kuwa kocha mpya. Uongozi wa timu ya Azam umemtangaza Iddi Nassor kuwa kocha mpya. Reviewed by Zero Degree on 12/30/2016 05:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.