Neema yazidi kutua msimbazi.
HUENDA msimu huu ukawa wenye mafanikio zaidi katika klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, baada ya viongozi na wadau wa Wekundu hao wa Msimbazi kuweka mikakati mbalimbali, ikiwemo ya ushindi pamoja na kuongeza kipato kwa klabu yao.
Simba, ambayo wiki hii ilifanya ziara mkoani Dodoma na kucheza mechi moja dhidi ya Polisi ya mjini humo na kupata ushindi wa mabao 2-0, ilipata nafasi ya kukutana na wabunge wanaoshabikia timu hiyo na kuweka mikakati mbalimbali ya ushindi.
Mkuu wa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, aliwaambia waandishi wa habari kwamba ziara yao ilikuwa ya mafanikio inayowapa matumaini makubwa ya kutwaa ubingwa msimu huu na pia kuboresha mipango ya kiuchumi ndani ya Simba.
Manara alisema, tayari klabu hiyo imeanza kufungua milango ya biashara ambapo kuanzia mechi ijayo ya Ligi Kuu kati ya Simba na Ruvu Shooting wataanza rasmi kuuza jezi mpya za klabu yao zitakazoingiza mapato klabuni.
Manara alisema, wanachama wao kutoka matawi mbalimbali nchini watafunguliwa fursa hiyo ili waweze kuuza jezi zao ili kujiongezea kipato na pia kuwapa nafasi wapenzi kununua bidhaa za klabu ili kuisaidia kimapato.
Simba leo itaingia katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kucheza mechi yake ya mzunguko wa tatu wa ligi hiyo ambapo katika mechi zilizopita timu hiyo ilipata ushindi wa mabao 3-1 na kisha ikapata matokeo ya suluhu ya 0-0 dhidi ya Ruvu JKT.

ZeroDegree.
Neema yazidi kutua msimbazi.
Reviewed by Zero Degree
on
12/07/2016 10:24:00 AM
Rating: