Loading...

Phiri kurejea kufumua na kuisuka upya klabu ya Mbeya City.

KOCHA wa Mbeya City, Mmalawi Kinnah Phiri anatarajiwa kurejea leo mjini Mbeya kuanza kuiandaa timu yake kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Phiri amekwama kurejea mapema kama alivyopanga kutokana na matatizo ya kifamilia na sasa atatua leo Mbeya.

Mapema wiki iliyopita akizungumza na Nipashe, Phiri alisema kwa sasa roho yake iko kwatu katika klabu hiyo kufuatia wachezaji kuanza kumuelewa na kuelewana pia.

“Niko sawa kwa sasa, sina malalamiko tena. Nafsi yangu iko vizuri, baada ya timu kuanza kukaa vizuri. Sasa nafikiria namna ya kujipanga kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu,”alisema.

Phiri alisema anatarajiwa kurejea Mbeya leo kutoka mapumzikoni Malawi, kufuatia kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.

Alisema anatarajia uongozi utakuwa umefanyia kazi mapendekezo yake ya usajili wa wachezaji wapya wa kuongeza nguvu katika mzunguko wa pili.

Mbeya City ilimaliza nafasi ya nane mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa pointi zake 19 za mechi 15, sawa na mahasimu wao wa Jiji la Mbeya, Prisons waliomaliza nafasi ya saba.

ZeroDegree.
Phiri kurejea kufumua na kuisuka upya klabu ya Mbeya City. Phiri kurejea kufumua na kuisuka upya klabu ya Mbeya City. Reviewed by Zero Degree on 12/05/2016 05:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.