Loading...

Sababu za ajali nyingi, matukio ya wizi na mauaji kutawala katika Mwezi Desemba.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Mohamed Mpinga.
“Nani kauona mwaka?” ni wimbo ulioimbwa na Bendi ya Sikinde, ambao una maana kubwa kutokana na vifo vinavyotokea mwishoni mwa mwaka.

Tukiwa tumebakiza siku 27 tuumalize mwaka 2016, Desemba umetajwa kuwa ni mwezi ulioghubikwa matukio ya uhalifu, ujambazi na vifo vitokanavyo na ajali na mauaji.

Desemba mwaka jana yaliripotiwa matukio kadhaa, ikiwamo ajali za mabasi ya abiria yaendayo mikoani ambayo yalisababisha watu wengi kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Pia, kumekuwapo na matukio ya uvamizi na uporaji wa mali ambayo huongezeka zaidi katika kipindi hicho cha mwisho wa mwaka.

Licha ya matukio hayo kuwa ni sehemu ya maisha ya kila siku, katika msimu wa mwisho wa mwaka ambao huambatana na sikukuu yamekuwa yakiongezeka kwa kile kinachoelezwa ni kutokana na ulevi, mwendokasi barabarani na kutafuta pesa kwa njia zisizo halali ili kutumia wakati wa sikukuu.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Sababu za ajali nyingi, matukio ya wizi na mauaji kutawala katika Mwezi Desemba. Sababu za ajali nyingi, matukio ya wizi na mauaji kutawala katika Mwezi Desemba. Reviewed by Zero Degree on 12/04/2016 09:03:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.