Siri ya Banda na Kocha Joseph Omog yafichuka.
BAADA ya kusota benchi kwa muda mrefu, kiraka wa Simba, Abdi Banda, anaamini mambo yatamwendea vizuri mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara, kwani tayari kocha wake, Joseph Omog amemwelewa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Banda alisema atahakikisha anaingia kwenye kikosi cha kwanza cha Wekundu hao baada ya mzunguko wa kwanza kuwa mbaya kwa upande wake.
Alisema anaamini kocha wa timu hiyo, Joseph Omog, hakupewa taarifa kamili kuhusiana na uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani, lakini baada ya kufanya hivyo ana uhakika atafanya makubwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
“Niko vizuri pia sichezi namba tatu tu, nina uwezo wa kucheza takribani nafasi nne, ukinipanga namba nne, tano na nane mimi freshi tu, mimi nazimudu kama ulivyoona kwenye mechi na Mtibwa,” alisema.
Banda alisema kusugua kwake benchi mzunguko wa kwanza hakuna maana kwamba alishuka kiwango, bali hiyo ilitokana na uwepo wa wachezaji wengi mahiri katika kikosi cha Simba kwa sasa.
“Najua kuna changamoto ya kuwania namba, ushindani ni mkubwa lakini juhudi zangu naamini zitanifanya nipate nafasi ya kuingia kikosi cha kwanza,” alisema.

Source: Bingwa
ZeroDegree.
Siri ya Banda na Kocha Joseph Omog yafichuka.
Reviewed by Zero Degree
on
12/18/2016 01:32:00 PM
Rating: