Loading...

Tevez akaribia kuwafunika wachezaji wote duniani kwa Mshahara mkubwa.

Jumapili hii mchezaji wa klabu ya soka ya Bocca Junior ya Argentina, Carlos Tevez alionekana kuwaaga mashabiki wake wa timu hiyo kuonyesha kuwa safari yake ya kuelekea kucheza kwenye ligi kuu ya China imeshaiva.

Mchezaji huyo ambaye anatarajia kukamilisha usajili wake wa kuhamia kwenye klabu ya Shangahi Shenhua inashiriki ligi kuu ya nchini China hivi karibuni ambayo imetangaza kumlipa mshahara wa paundi laki sita ikiwa ni sawa na kiasi cha shilingi 1.8 bilioni kwa fedha za Tanzania.

Tevez atakuwa ndio mchezaji anayelipwa fedha nyingi duniani endapo dili hilo litakamilika na kuzidi dau aliloahidiwa kiungo wa Chelsea la kulipwa mshahara wa paundi laki nne kwa wiki na klabu ya Shanghai SIPG.

ZeroDegree.
Tevez akaribia kuwafunika wachezaji wote duniani kwa Mshahara mkubwa. Tevez akaribia kuwafunika wachezaji wote duniani kwa Mshahara mkubwa. Reviewed by Zero Degree on 12/20/2016 05:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.