Loading...

Ridhiwani Kikwete ampongeza msanii Belle 9 kwa kutoa wimbo mzuri.

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amempongeza msanii Belle 9 kwa kutoa wimbo mzuri mpya, 'Give It To Me' na akamtaka kuendeleze juhudi hizo ili afanikiwe zaidi kimuziki.

Akizungumza Jumamosi usiku katika sherehe ya uzinduzi wa video ya wimbo huo uliofanyika nyumbani kwa Kikwete, eneo la kingo za Bahari, Kawe jijini Dar es Salaam, Mbunge huyo kijana alimsifu Belle 9 kwa kutoa wimbi bora wenye hadhi ya kimataifa. 

Pamoja na hayo, Ridhiwani ambaye ni shabiki mkubwa wa Yanga, akamtaka msanii huyo kutotosheka mapema na mafanikio hayo madogo, badala yake kuongeza juhudi na ubunifu ili atoe kazi nzuri zaidi.

“Huu wimbo tumekuja kuuona hapa leo, kwa kweli ni mzuri na mimi binafsi ninaupa sifa zote za kimataifa. Lakini pamoja na kumpongeza Belle 9 kwa kazi hii nzuri, ninamsihi tu asivimbe kichwa, badala yake aongeze ubunifu ili afanye kazi nzuri zaidi,”alisema.

Kwa upande wake, Belle 9 alisema ameupokea ushauri wa Ridhiwani na ataufanyia kazi kuhakikisha anaendelea kufanya vizuri kwenye medani ya muziki.

Katika wimbo huo, Belle 9 kamshirikisha G Nako na video imetengezwa na mtayarishaji maarufu, Nicolas wa Afrika Kusini.

ZeroDegree.
Ridhiwani Kikwete ampongeza msanii Belle 9 kwa kutoa wimbo mzuri.  Ridhiwani Kikwete ampongeza msanii Belle 9 kwa kutoa wimbo mzuri. Reviewed by Zero Degree on 12/20/2016 05:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.