Loading...

VIDEO: Bodi ya mikopo [HESLB] kuwabana waajiri wasiowasilisha makato na majina ya wanufaikaji wa mikopo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul Razaq Badru.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), Abdul Razaq Badru ameunda kikosi maalumu (Task force) kwa ajili ya msako wa kuwanasa waajiri sugu wote nchini wasiowasilisha makato na majina ya wanufaikaji wa mikopo ya bodi hiyo.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Badru amesema kikosi kazi hicho kitaanza kazi Januari 2, mwaka 2017 na kitafanya kazi hiyo kwa siku 14 mfululizo wakipita ofisi moja baada ya nyingine.

Amesema wadaiwa sugu ni wale walioshindwa kurejesha kwa kipindi cha zaidi ya miaka 10. Kiasi kilichokusanywa na Bodi hiyo hadi sasa ni Sh 140bilioni kati ya Sh300bilioni na deni linalodaiwa ni Sh160bilioni.



ZeroDegree.
VIDEO: Bodi ya mikopo [HESLB] kuwabana waajiri wasiowasilisha makato na majina ya wanufaikaji wa mikopo. VIDEO: Bodi ya mikopo [HESLB] kuwabana waajiri wasiowasilisha makato na majina ya wanufaikaji wa mikopo. Reviewed by Zero Degree on 12/28/2016 07:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.