Loading...

VIDEO: Jinsi Liverpool walivyoadhibiwa vilivo na vijana wa Bournemouth.

Liverpool ndiyo timu ambayo iilikuwa ikiwafukuzia kwa ukaribu Chelsea katika mbio za kuwania ubingwa msimu huu ambao ndio vinara katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza. 

Baada ya kuwashuhudia The Blues wakiibuka na ushindi ugenini dhidi ya Manchester City, walikuwa wanatambua wanalazimika kupata pointi zote tatu dhidi ya Bournemouth ili kupunguza gape la points.

Kikosi hicho cha Jurgen Klopp kilikuwa mbele kwa magoli 2-0 kabla ya kupoteza uongozi wao hatimaye kupoteza mchezo.

Magoli ya AFC Bournemouth yalifungwa na Callum Wilson dakika ya 56 kwa penati, Ryan Fraser dakika ya 76, Steve Cook dakika ya 79 na Nathan Ake dakika ya 90, huku Liverpool walianza kupata goli mapema tu dakika ya 20 kupitia Sadio Mane, Divock Origi dakika ya 22 na Emre Can dakika ya 64.

Kama ni shabiki wa Liverpool najua utakuwa umesikitishwa na goli la dakika za lala salama la AFC Bournemouth lililofungwa dakika ya 90 ya mchezo na kuifanya Liverpool kutoka uwanjani vichwa chini kwa kufungwa jumla ya goli 4-3.



ZeroDegree.
VIDEO: Jinsi Liverpool walivyoadhibiwa vilivo na vijana wa Bournemouth. VIDEO: Jinsi Liverpool walivyoadhibiwa vilivo na vijana wa Bournemouth. Reviewed by Zero Degree on 12/05/2016 04:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.