Loading...

Mchezaji wa Mbao FC afariki uwanjani baada ya kugongana na beki wa Mwadui.

MSHAMBULIAJI wa timu ya vijana ya Mbao, Khalfan Ismail, amefariki dunia, baada ya kugongana na kuanguka uwanjani katika mchezo wa michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 20.

Mchezo huo ulipigwa jana kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, mkoani Kagera ambako michuano hiyo inaendelea.

Mchezaji huyo aligongana na beki wa Mwadui wakati wakiwa katika harakati ya kuwania mpira na kuanguka na juhudi za kuokoa maisha yake zilionekana kugonga mwamba.

Baadaye mchezaji huyo alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Kagera, lakini wakati tunakwenda mitamboni, taarifa zilizotufikia zilieleza kuwa Ismail alifariki wakiwa uwanjani.

ZeroDegree.
Mchezaji wa Mbao FC afariki uwanjani baada ya kugongana na beki wa Mwadui. Mchezaji wa Mbao FC afariki uwanjani baada ya kugongana na beki wa Mwadui. Reviewed by Zero Degree on 12/05/2016 04:44:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.