Loading...

Wabunge Korea kusini wapiga kura kumuondoa Rais Madarakani.

Waandamanaji wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Seoul wakitaka Bi Park aondolewe madarakani.
Wabunge nchini Korea Kusini wamepiga kura kumuondoa madarakani Rais wa Park Geun-hye.

Hoja hiyo imepitishwa na wabunge 234 dhidi ya 56.

Maelfu ya waandamanaji walikuwa wamekusanyika nje ya majengo ya bunge mjini Seoul wakitaka Bi Park aondolewe madarakani.

Hatua hiyo itamlazimisha Bi Park kung'atuka kwa muda huku Mahakama ya Kikatiba ikiamua iwapo ataondolewa kabisa kutoka wadhifa huo wa urais.

Suala kuu limekuwa ni uhusiano kati ya Bi Park na msiri wake mkuu Choi Soon-sil, ambaye anadaiwa kutumia uhusiano huo kujizolea ushawishi nchini humo.

Viongozi wa mashtaka wanasema Bi Park alikuwa na "mchango mkubwa" katika visa kadha vya ufisadi, tuhuma ambazo amezikanusha.

Aidha, alikataa wito wa kumtaka ajiuzulu akisema uamuzi huo aliuachia bunge.

Bi Park amekataa wito wa kumtaka ajiuzulu.
Bunge la Korea Kusini lilianzisha hoja hiyo Alhamisi, ambapo iilihitaji kuungwa mkono na angalau theluthi mbili ya wabunge ndipo kupitishwa.

Wachanganuzi walikuwa wanasema hilo lingekuwa jambo ngumu.

Bunge linatawaliwa na vyama vya upinzani na wabunge huru ambao wanataka aondolewe madarakani, lakini walihitaji wabunge 28 zaidi kutoka kwa chama cha Saenuri, chake Bi Park, ndipo wafikishe idadi ya kura inayohitajika.

Lakini matokeo yanaonesha wapo wabunge wa chama chake waliompinga.

Bi Choi ni rafiki wa karibu wa Bi Park.
ZeroDegree.
Wabunge Korea kusini wapiga kura kumuondoa Rais Madarakani. Wabunge Korea kusini wapiga kura kumuondoa Rais Madarakani. Reviewed by Zero Degree on 12/09/2016 03:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.