Loading...

Yanga sasa hali tete, ..wachezaji waendeleza mgomo.

kocha mkuu, George Lwandamina.
MGOMO ulioanza juzi Jumatatu kwa wachezaji wa Yanga umeendelea tena jana kwa kile kilichoelezwa kushinikiza uongozi kuwalipa mishahara yao.

Hali hiyo huenda ukazifaidisha zaidi timu pinzani kwenye mbio za ubingwa hususan Simba inayoongoza ligi kwa sasa kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya Yanga yenye pointi 36.

Mgomo huo jana uliendelea kufanyika ikiwa ni siku tatu tu kabla ya mchezo wao wa pili wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu dhidi ya African Lyon.

Jana asubuhi kocha mkuu, George Lwandamina alifika uwanjani kama kawaida kwa ajili ya mazoezi, lakini wachezaji wake wachache waliohudhuria hawakuonyesha kujali wala kuwa na hofu kwa kugomea mazoezi hayo.

Lwandamina alilazimika kufuta mazoezi hayo ambapo pamoja na kufika uwanjani wachezaji wa Yanga hawakushuka kwenye basi lao.

Mmoja wa wachezaji wa timu hiyo ambaye hakuwa tayari jina lake kutajwa gazetini, alisema wanashinikiza kulipwa mshahara wao wa Novemba ili waweze kujikimu na familia zao kwenye kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

"Kocha ameelewa malalamiko yetu na tumemwambia nini tunachotaka, tunasubiri viongozi nini wataamua," alisema mchezaji huyo.

Hata hivyo, kwa upande wa Kaimu Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deusdedit alikiri kuwapo kwa tatizo hilo la kutolipwa mshahara wa mwezi uliopita na kuelezea kuwa linashughulikiwa na kwamba watalipa muda wowote kuanzia sasa kabla ya mechi hiyo ya Ijumaa.

"Hili suala tutalitatua, uongozi unafanyia kazi na muda wowote kuanzia sasa tutalimaliza, hivyo kila kitu kitakuwa sawa kuelekea mechi ijayo," alisema Baraka.

ZeroDegree.
Yanga sasa hali tete, ..wachezaji waendeleza mgomo. Yanga sasa hali tete, ..wachezaji waendeleza mgomo. Reviewed by Zero Degree on 12/21/2016 12:43:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.