Loading...

Afcon: Gabon wapata sare ya 3 mfuluizo, ..waweka rekodi ya wenyeji kutolewa nje mapema

Pierre-Emerick Aubameyang akisikitika jana baada ya kukosa bao la wazi mapema tu
HUZUNI kwa wenyeji, Gabon baada ya kutolewa kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kufuatia sare ya bila kufungana na Cameroon mjini Libreville.

Nyota Pierre-Emerick Aubameyang alikosa bao la wazi mapema tu wakati Denis Bouanga aliaanguka chini na kuangua kilio baada ya kugongesha nguzo dakika za mwishoni, hiyo ikiwa sare ya tatu mfululizo katika mechi zao nyingi.

Na kwa sare hiyo pamoja na zile mbili za 1-1 dhidi ya Burkina Faso na Guinea-Bissau katika mechi za awali, Gabon inamaliza na pointi tatu na inaaga mashindano, wakiweka rekodi ya kuwa wenyeji wa nne na wa kwanza tangu Tunisia mwaka 1994 kutolewa hatua ya makundi.

Kwa pointi saba, Cameroon wanakwenda Robo Fainali kama vinara wa Kundi A wakifuatiwa na Burkina Faso ambayo jana iliifunga 2-0 Guinea-Bissau mjini Franceville.

Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi za Kundi B, Zimbabwe ya Bruce Kangwa wa Azam FC ikimenyana na Tunisia Uwanja wa d'Angondje na Senegal ikimenyana na Algeria Uwanja wa Franceville mechi zote zikianza Saa 4:00 usiku.

ZeroDegree.
Afcon: Gabon wapata sare ya 3 mfuluizo, ..waweka rekodi ya wenyeji kutolewa nje mapema Afcon: Gabon wapata sare ya 3 mfuluizo, ..waweka rekodi ya wenyeji kutolewa nje mapema Reviewed by Zero Degree on 1/23/2017 11:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.