Loading...

Anglikana wamwandalia adhabu Askofu Mokiwa

Askofu Valentino Mokiwa 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana nchini, Jacob Chimeledya amesema watachukua hatua zaidi dhidi ya Askofu Valentino Mokiwa wa kanisa hilo Dayosisi ya Dar es Salaam kwa kuwa bado anaendelea kutoa huduma licha ya kutakiwa kujiuzulu.

Wiki tatu zilizopita Mokiwa aliandikiwa barua na Askofu Chimeledya akitakiwa kujiuzulu akidaiwa kuvunja miiko ya kanisa hilo na kutumia madaraka yake vibaya ikiwamo kufanya ubadhirifu wa fedha.

Hata hivyo, Dk Mokiwa amekuwa akikana tuhuma dhidi yake akisema mgogoro wa kanisa hilo ni wa kutengenezwa na adui zake.

Akizungumza kwa simu jana, Askofu Chimeledya hakuzitaja hatua zitakazochukuliwa dhidi ya Askofu Mokiwa, akisema hakuna ulazima wa kuziweka hadharani hadi pale zitakapochukuliwa na kanisa hilo.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Anglikana wamwandalia adhabu Askofu Mokiwa Anglikana wamwandalia adhabu Askofu Mokiwa Reviewed by Zero Degree on 1/23/2017 11:29:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.