Loading...

Afcon: Mabingwa watetezi, Ivory Coast waponea chupchupu kwa DRC wakati Togo ikichapwa 3 [Video]

MABINGWA watetezi, Ivory Coast wamenusurika kuchapwa na Jamhuri ya Kidemkrasia ya Kongo (DRC) baada ya kupambana na kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kupata sare ya 2-2 katika mchezo wa Kundi C Kombe la Mataifa ya Afrika usiku huu Uwanja wa d'Oyem.
Kwa matokeo hayo, DRC inaendelea kuongoza Kundi C ikifikisha pointi nne, wakati mabingwa watetezi, Ivory Coast wanateremka hadi nafasi ta tatu, nyuma ya Morocco yenye pointi tatu na Togo inashika mkia kwa pointi yake moja.

Mabao ya DRC yamefungwa na Neeskens Kebano dakika ya 10 na Junior Kabananga dakika ya 29, wakati ya Ivory Coast yamefungwa na Wilfried Bony dakika ya 26 na Serey Die dakika ya 67.

Kikosi cha Ivory Coast kilikuwa: Gbohouo; Aurier, Kanon, Bailly, Traore/Del dk46, Doukoure, Kessie, Serey Die, Zaha, Bony na Gradel/Kalou dk77.



DRC: Matampi; Ikoko/Mulumbu dk72, Tisserand, Mbemba, Issama, Maghoma/Mulumba dk72, Bope; Mubele, Kebano, Kage na Mbokani.

Katika mchezo wa usiku, Morocco imeibamiza mabao 3-1 Togo. Mabao ya Morocco yamefungwa na Aziz Bouhaddouz dakika ya 15, Romain Saiss dakika ya 21 na Youseff En-Nesyri dakika ya 72, wakati la Togo limefungwa na Matthieu Dossevi dakika ya tano.

Kwa mara nyingine, beki wa Yanga, Vincent Bossou alikuwa benchi kwa dakika zote 90 kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza, Togo wakilazimishwa sare ya 0-0 na Ivory Coast.

Michuano hiyo itaendelea Jumamosi kwa michezo ya Kundi D kati ya Ghana na Mali Saa 1:00 usiku na Misri na Uganda Saa 4:00 usiku.



ZeroDegree.
Afcon: Mabingwa watetezi, Ivory Coast waponea chupchupu kwa DRC wakati Togo ikichapwa 3 [Video] Afcon: Mabingwa watetezi, Ivory Coast waponea chupchupu kwa DRC wakati Togo ikichapwa 3 [Video] Reviewed by Zero Degree on 1/21/2017 09:32:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.