Loading...

Afcon: Misri watinga nusu fainali baada kuifunga Morocco, ...ratiba kamili ya nusu fainali iko hapa.

BAO la dakika ya 87 la Mahmoud Kahraba jana limetosha kuipeleka Nusu Fainali Misri baada ya kuilaza 1-0 katika Robo Fainali ya mwisho ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mjini Port-Gentil, Gabon.

Kahraba alifunga bao hilo baada ya kukutana na mpira uliomgonga Ahmed Hassan kufuatia kona na kuusukumia nyavuni kiulaini na kuzima ndoto za kocha wa Morocco, Mfaransa Herve Renard kutwaa taji la tatu la AFCON.

Ushindi huo wa kwanza kwa Mafarao wa Misri dhidi ya wapinzani wao hao wa Kaskazini mwa Afrika baada ya zaidi ya miaka 30 unawafanya wakutane na Burkina Faso kwenye Nusu Fainali  saa 4:00 usiku wa Jumatano, wakati Ghana itamenyana na Cameroon saa 4:00 usiku wa Alhamis.

ZeroDegree.
Afcon: Misri watinga nusu fainali baada kuifunga Morocco, ...ratiba kamili ya nusu fainali iko hapa. Afcon: Misri watinga nusu fainali baada kuifunga Morocco, ...ratiba kamili ya nusu fainali iko hapa. Reviewed by Zero Degree on 1/30/2017 11:39:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.