Loading...

Afcon: Senegal yatinga robo fainali moja kwa moja, ..wakati Tunisia ikijipatia ushindi wake wa kwanza [Video]

Baada ya jioni ya January 19 2017 kushuhudia mchezo wa kwanza wa Kundi B katika uwanja wa Franceville ukizikutanisha timu za Tunisia dhidi ya Algeria na kushuhudia Tunisia ikiibuka kidedea kwa ushindi wa goli 2-1, usiku wake ilikuwa ni zamu ya Senegal kuivaa Zimbabwe.

Mchezo wa pili wa kati ya Senegal dhidi ya Zimbabwe umedhihirisha safari ya Senegal kuingia moja kwa moja hatua ya robo fainali, hiyo ni baada ya ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Zimbabwe, magoli ambayo yalifungwa na Sadio Mane dakika ya 9 na Henri Saivet aliyefunga goli dakika ya 14 kwa mpira wa adhabu ndogo.



Ushindi huo umeifanya Senegal kutinga hatua ya robo fainali kwa kufikisha jumla ya point sita huku wakisalia na mchezo mmoja, Senegal anaongoza Kundi B kwa kuwa na point 6, wakifuatiwa na Tunisia wenye point tatu, Algeria na Zimbabwe wakiwa nafasi ya tatu na nne kwa kuwa na point moja moja kila mmoja huku wakiwa wamepishana magoli yakufunga na kufungwa.


Michuano hiyo inaendelea tena leo kwa mechi za Kundi C, wenyeji Ivory Coast ikimenyana na D.R. Congo kuanzia Saa 1:00 usiku na Morocco ikimenyana na Togo kuanzia Saa 4:00 usiku.
ZeroDegree.
Afcon: Senegal yatinga robo fainali moja kwa moja, ..wakati Tunisia ikijipatia ushindi wake wa kwanza [Video] Afcon: Senegal yatinga robo fainali moja kwa moja, ..wakati Tunisia ikijipatia ushindi wake wa kwanza [Video] Reviewed by Zero Degree on 1/20/2017 11:03:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.