Loading...

Afcon: Uganda yaaga rasmi mashindano, wakati Gyan akiipeleka Ghana robo finali [Video]

MSHAMBULIAJI Asamoah Gyan ameipeleka Ghana Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika huku Uganda ikiwa timu ya kwanza kuhakikishiwa safari ya kurejea nyumbani baada ya hatua ya makundi.

Gyan alifunga bao pekee katika mchezo wa kwanza wa Kundi D dakika ya 21 akimalizia krosi ya Jordan Ayew, Black Stars ikiilaza 1-0 Mali.

Misri ikaitupa nje Uganda kwa bao pekee la mtokea benchi Abdallah El Said dakika ya 89.



Ghana ambao pia ni washindi wa pili wa mwaka 2015 wanakuwa timu ya pili kujihakikishia Robo Fainali hadi sasa baada ya Senegal.

Michuano hiyo inaendelea leo kwa wenyeji Gabon kumenyana na Cameroon katika mchezo wa Kundi A mjini Libreville ambao wanatakiwa lazima washinde ili kwenda Robo Fainali.

Wakifungwa watatolewa na wakitoa sare itabidi wasikilizie matokeo ya mechi nyingine ya mwisho ya kundi hilo kati ya Burkina Faso na Guinea-Bissau.

Rais wa Gabon, Ali Bongo aliwatembelea wachezaji jana na kipa Didier Ovono akasema: "Rais ametupa hamasa kuelekea mechi hiyo. Hiyo itakuwa fainali yetu ya kwanza."

ZeroDegree.
Afcon: Uganda yaaga rasmi mashindano, wakati Gyan akiipeleka Ghana robo finali [Video] Afcon: Uganda yaaga rasmi mashindano, wakati Gyan akiipeleka Ghana robo finali [Video] Reviewed by Zero Degree on 1/22/2017 11:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.