Loading...

Dk Abdallah Possi ajiuzulu ubunge

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu aliyekuwa akishughulikia Walemavu, Dk Abdallah Possi amemuandikia Spika wa Bunge barua ya kujiuzulu.

Uamuzi huo wa Dk Possi umekuja siku tatu baada ya Rais John Magufuli kumteua kuwa balozi.

Spika wa Bunge, Job Ndugai alithibitisha kupokea barua ya kujiuzulu ya mbunge huyo jana na kueleza kuwa nafasi yake imebaki wazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bunge, Spika Ndugai tayari amemuandikia barua Rais kumfahamisha juu ya kujiuzulu kwa Dk Possi kama mbunge wa kuteuliwa.


Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Dk Abdallah Possi ajiuzulu ubunge Dk Abdallah Possi ajiuzulu ubunge Reviewed by Zero Degree on 1/22/2017 11:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.