Loading...

Alichosema Michael Ballack juu ya nahodha wa Chelsea, John Terry

Kiungo wa zamani wa Chelsea, Michael Ballack hana uhakika tena ni kiasi gani na kwa muda gani John Terry anaweza kuendelea kupigania nafasi yake akiwa Stamford Bridge.

Kiungo huyo wa zamani wa 'The Blues' alihudhuria mazoezi ya klabu yaliyofanyika Cobham wiki hii.

Ballack anamfahamu vizuri sana John Terry tangu walipokuwa pamoja magharibi ya London, na anaujuau ushawishi wa Terry kikosini.

Ballack anakisia kwamba mazoezi kwa walinzi wa kati wa klabu ya Chelsea yanaweza kuwa yamebadilika na kuwa katika ubora sana.

"Yeye ni mkubwa, huwezi kuzungumzia ushawishi wake katika miaka mingi zaidi iliyopita na bila kusahau utu wake," Ballack aliiambia Chelsea TV.

"Sasa ni hatua ambapo yeye amefikia umri ambapo ana uwezo wa kuamua ni kwa muda gani anaweza kuendelea katika ngazi ile, kwa sababu niliaona mazoezi yao ni makali kabisa na sidhani kama ni rahisi kwa mtu wa umri wake.

"Hata hivyo, hadhi yake bado iko pale pale, ubora uko pale pale na inaonekana kuwa yeye anafuraha.


"Na kwa muda ambapo wewe unakuwa na furaha kama mchezaji unataka kuwa sehemu ya timu, na kwenda nao katika mazoezi kuwasaidia wengine kwa uzoefu wako.

"Yeye anaonekana kufanya hivyo." Alisema Ballack.

ZeroDegree.
Alichosema Michael Ballack juu ya nahodha wa Chelsea, John Terry Alichosema Michael Ballack juu ya nahodha wa Chelsea, John Terry Reviewed by Zero Degree on 1/20/2017 10:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.