Loading...

Aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza afariki dunia

Graham Taylor
Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Graham Taylor amefariki dunia,Graham ambae ameshawahi kuwa kocha wa vilabu kama Aston Villa na Watford amefariki akiwa na umri wa miaka 72.

Taylor alizaliwa mwaka 1944 huko Worksop na kupata mafanikio katika soka akiwa kama mchezaji wa timu ya Lincoln City aliiongoza Uingereza kwenye fainali za mataifa Ulaya za mwaka 1992 huko Sweden kabla ya kujiuzulu ukocha mwaka 1994 baada ya England kushindwa kufuxu kombe la dunia.

Mwaka 1994 Taylor alifanikiwa kuipeleka timu ya Watford kwenye fainali za kombe la FA na kuambulia kipigo cha goli mbili kwa sifuri kutoka Everton baada ya hapo Taylor alihamia Aston Villa,katika taarifa iliyotolewa na familia yake mchana huu inasema “tukiwa na majonzi makubwa tunawafahamisha kifo cha Graham kilichotokea leo kutokan na ugonjwa wa moyo(heart attack)”

Chama cha soka Uingereza nacho kupitia ukurasa wao wa twitter walieleza majonzi yao juu ya kifo cha Graham,Watford nao waliandika kwenye ukurasa wao wa twitter “kila mmoja wetu ana majonzi juu ya kifo chako,tunakupenda Taylor”.

Mwaka 1992 Graham aliingia kwenye mzozo na mashabiki wa Uingereza na vyombo vya habari baada ya kumtoa mshambuliaji wao Garry Lineker ambae sasa ni mchambuzi wa soka katika mechi ambayo Uingereza ilikuwa ikihitaji goli la ushindi katika ukurasa wa twitter Allan Shearer nae ameandika “nimepatwa na mshtuko mkubwa,ni kocha wa kwanza kuniamini Uingereza,nimesikitika”

ZeroDegree.
Aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza afariki dunia Aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Uingereza afariki dunia Reviewed by Zero Degree on 1/13/2017 11:34:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.