Loading...

Barcelona yafanya kweli Ligi Kuu ya Hispania, ..Messi aweka rekodi mpya

Barcelona imeendelea kuwasogelea mahasimu wao Real Madrid ambao wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Hispania baada ya kuibuka na ushindi wa magoli matano bila dhidi ya Las Palmas, mchezo uliopigwa katika dimba la Camp Nou.

Katika mchezo huo, magoli ya Barcelona yamefungwa na Luis Suarez dakika ya 14 na 57, Lionel Messi dakika ya 52, Arda Turan 59 na Aleix Vidal ushindi ambao umeiwezesha Barcelona kufikisha alama38 nyuma kwa alama mbili dhidi ya Real Madrid yenye alama 40 huku wakiwa na tofauti ya michezo miwili.

Pamoja na ushindi ambao Barcelona imeupata pia umemwezesha staa wa timu hiyo, Lionel Messi kuweka rekodi ya kuwa mchezaji ambae amezifunga timu zote ambazo zimewahi kushiriki Ligi Kuu ya Hispania ambazo ni 35.

ZeroDegree.
Barcelona yafanya kweli Ligi Kuu ya Hispania, ..Messi aweka rekodi mpya Barcelona yafanya kweli Ligi Kuu ya Hispania, ..Messi aweka rekodi mpya Reviewed by Zero Degree on 1/15/2017 01:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.