Loading...

Drogba kuhamia klabu hii ya Nchini Brazil

Mshambuliaji wa kimataifa wa zamani wa Ivory Coast Didier Drogba, 38, yuko katika mazungumzo ya kuhamia klabu ya Brazil ya Corinthians Paulista, gazeti la Jeune Afrique limeripoti.

Drogba hajahusishwa na klabu yoyote tangu mwezi Disemba alipoiaga klabu ya Impact de Montreal ya Canada.
Kwa hivi sasa ana matarajio ya kujiunga na klabu ya Corinthians Paulista kwa msimu wa 2017.

Raia huyo kutoka Ivory Coast alitaka kurudi Olympique de Marseille ambapo alipata umaarufu msimu wa 2003-2004, lakini kocha Rudi Garcia hakuunga mkono pendekezo hilo, Gazeti hilo la Paris limeripoti.

Gazeti hilo la Jeune Afrique limemnukuu Drogba akisema: ''Kwa hivi sasa, mazungumzo yamekuwa yakiendelea kuhusiana na klabu ya Brazil ya Corithians kwa mkataba wa miezi sita hadi 12." Drogba amekuwa akisubiri majibu ambayo yanaonekana kuwa mazuri'.

Drogba alitangaza kustaafu kwake kutoka kwa soka ya kimataifa miaka miwili iliyopita.

Mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea alifunga magoli 65 katika mechi 104 alizoshiriki kwenye timu ya taifa Ivory Coast kwa miaka 12.

Amechezea michuano ya kombe la kimataifa mara tatu.

ZeroDegree.
Drogba kuhamia klabu hii ya Nchini Brazil Drogba kuhamia klabu hii ya Nchini Brazil Reviewed by Zero Degree on 1/17/2017 11:02:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.