Loading...

Hiki ndicho alichosema Msuva kwa wale wanaomlilia Donald Ngoma

WAKATI mashabiki wa Yanga wakiwa na hofu ya kumkosa mshambuliaji wao matata Mzimbabwe, Donald Ngoma, katika mchezo wa leo dhidi ya Majimaji,mtambo wa mabao, Amissi Tambwe na winga hatari, Simon Msuva, wameahidi kufanya mauaji katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa Uwanja wa Majimaji, mjini Songea, Ruvuma.

Wawili hao wapo kileleni katika orodha ya wachana wavu,wakiingia kimiani mara tisa kama ilivyo kwa winga wa Simba, Shiza Kichuya.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Msuva alisema japo uwapo wa Ngomakatika kikosi chao ni muhumu, lakini watapambana vilivyo kupata pointi tatu bila ya mwenzao huyo.

“Naamini kwauwiano mzuri uliopokikosini tutafanya vizuri licha ya kukosa huduma ya mwenzetu Donald Ngoma… tuna nafasi kubwa ya kuwanyamazisha wapinzani wetu,” alisema Msuva akiungwa mkono na Tambwe.

Source: Bingwa
ZeroDegree.
Hiki ndicho alichosema Msuva kwa wale wanaomlilia Donald Ngoma Hiki ndicho alichosema Msuva kwa wale wanaomlilia Donald Ngoma Reviewed by Zero Degree on 1/17/2017 10:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.