Loading...

Ibrahimovic akerwa na kiwango cha Manchester United

Licha ya mchezo wa mahasimu wa Ligi Kuu ya Uingereza Man United na Liverpool kumalizika kwa sare ya goli 1-1 hilo halijamzuia mshambualiaji wa Man United, Zlatan Ibtamovic kuzungumza kuhusu kiwango ambacho kimeonyeshwa na timu yake na kushindwa kuibuka na ushindi na kuendeleza rekodi yao ya kushinda michezo tisa mfululizo.

Ibrahimovic alisema kuwa mchezo wa Liverpool hawakuwa katika kiwango kizuri na walicheza vibaya huku wakifanya makosa mengi katika kipindi cha kwanza hali iliyopelekea Liverpool kupata goli lakini kama vipindi vyote wangecheza kama kipindi cha pili basi anaamini matokeo yangekuwa tofauti.
“Tumepata alama moja, lakini hatukuwa katika kiwango chetu bora, ni mchezo mgumu, tulikuwa nyuma na walikuwa wakitukimbiza lakini hadi mwisho tulikuwa sawa,” alisema Ibrahimovic na kuongeza.

“Tulifanya makosa ya kawaida sana. Hatukuwa vizuri sababu ya kasi ya mchezo ya wapinzani wetu na ninaamini tulicheza vibaya, kama kipindi cha kwanza tungecheza kama ilivyokuwa kipindi cha pili ungekuwa ni mchezo wa tofauti.”

ZeroDegree.
Ibrahimovic akerwa na kiwango cha Manchester United Ibrahimovic akerwa na kiwango cha Manchester United Reviewed by Zero Degree on 1/17/2017 10:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.