Loading...

Zlatan Ibrahimovic ashinda kesi juu ya tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.

Zlatan Ibrahimovic alipokuwa na klabu ya Juventus
STOCKHOLM (AP), mahakama ya Kiswidish imempiga faini aliyekuwa kocha wa zamani wa nchi ya Sweden kufuatia kumshutumu Zlatan Ibrahimovic kuhusika na utumiaji wa madawa ya kulevya wakati akiwa Juventus.

Mahakama ya Wilaya ya Varmland imemtaka kocha huyo kulipa faini ya 24,000 kronor  ya Sweden, sawa na dola za kimarekani 2,650 kwa kumkashifu mshambuliaji wa Manchester United katika maoni aliyoyatowa wakati wa mjadala mmoja ivi uliofanyika mwaka jana.


Karlsson alisema, bila kutoa vielelezo/uthibitisho, kwamba alikuwa "anaamini" kuwa Ibrahimovic alitumia dawa hizo kwa sababu alipata ongezeko la "kilo 10 za misuli" ndani ya mwaka mmoja wakati akiwa Juventus. Yeye alitoa hoja hizo sawa na gazeti moja la nchini humo.

Ingawa Karlsson baadaye alimuomba msamaha Ibrahimovic, lakini mshambuliaji huyo wa Sweden alimshitaki kwa kumkashifu.

Ibrahimovic, ambaye hajawahi kubainika katika vipimo chanya vya watumiaji wa madawa hayo, aliichezea klabu ya Juventus kuanzia 2004 hadi 2006.

ZeroDegree.
Zlatan Ibrahimovic ashinda kesi juu ya tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya. Zlatan Ibrahimovic ashinda kesi juu ya tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya. Reviewed by Zero Degree on 1/10/2017 06:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.