Ibrahimovic awanyamanzisha waliomponda
ULE ugonjwa ulioisumbua klabu ya Manchester United kabla ya ujio wa wachezaji wapya sasa umetibika. Ni baada ya kumnyakua bure mshambuliaji, Zlatan Ibrahimovic, katika dirisha kubwa la usajili wa mwaka jana, Msweden aliyepitia ligi mbalimbali barani Ulaya na kuichezea miamba kadhaa ya soka barani humo.
United ya sasa imerudi kwenye ukali wao wa kupachika mabao ambapo mtu anayeifanya kazi hiyo kwa ufasaha ni Ibrahimovic.
Msimu uliopita, United haikuwa na safu kali ya ushambuliaji ambayo iliwategemea mastraika hawa; Wayne Rooney, Anthony Martial au Marcus Rashford, ambao walifunga mabao machache mno.
Ujio wa Zlatan umepandisha takwimu ya mabao pale United, kwa kile alichokifanya Ligue 1 ya Ufaransa ambayo ni ligi yake ya mwisho kuichezea kabla ya kutua England ndani ya klabu ya PSG kwa kukabiliana vilivyo na mastraika wengine wenye uwezo mzuri wa kupachika mabao kama Edinson Cavani, Alexandre Lacazette ni wazi United wamekula dume kwa Msweden huyo.
Hadi sasa mshambuliaji huyo ameshadhihirisha kuwa ni usajili bora kabisa uliofanywa na Man United, kwa kufanya mambo makubwa kuliko washambuliaji wengine ndani ya klabu hiyo kwa kipindi cha misimu miwili iliyopita.
Watu wengi hawakuamini kama Zlatan, 35, angeweza kuendelea na kazi yake ya ufungaji kwa kile kilichoonekana kuwa ni hofu ya umri wake kuwa mkubwa na kukosa uzoefu wa kucheza kwenye Ligi Kuu England, lakini amewanyamazisha wale wote waliokuwa wakiponda usajili wake.
Hadi sasa mshambuliaji huyo ametupia jumla ya mabao 18 katika michuano yote msimu huu, hiyo ikiwa na maana kwamba Zlatan amempiku Anthony Martial aliyefunga jumla ya mabao 17 na kumaliza msimu uliopita kama mfungaji bora wa klabu hiyo.
Msimu mmoja kabla ya Martial kung’ara, nahodha Wayne Rooney, pia alifanya vizuri kwa kufunga mabao 14 katika michuano yote lakini rekodi hiyo ya mabao ilifikiwa na Zlatan na kudhihirisha kuwa yeye ni mtu wa muhimu aliyetakiwa kuwepo United baada ya miaka kadhaa ya klabu kusota chini ya Louis van Gaal.
Bao moja alilofunga usiku wa kuamkia jana dhidi ya West Ham katika ushindi wa mabao 2-0, ndilo lililomsaidia kufikisha mabao hayo 18 na kuifanya timu yake ya United kuibuka na ushindi wao wa sita mfululizo wa Ligi Kuu England.
Unaikumbuka silaha ya Jose Mourinho kule Inter Milan, ndiyo hii aliyonayo katika dimba la Old Trafford, ni Zlatan Ibrahimovic.

ZeroDegree.
Ibrahimovic awanyamanzisha waliomponda
Reviewed by Zero Degree
on
1/04/2017 12:22:00 PM
Rating: