Loading...

Aliyetekeleza shambulizi lililoua watu 39 Istanbul akamatwa

Abdulkadir baada ya kukamatwa
Vyombo vya habari nchini Uturuki vimesema mshukiwa mkuu katika shambulizi la mkesha wa mwaka mpya mjini Istanbul amekamatwa.

Abdulkadir Masharipov anaaminika kufanya shambulizi hilo ambalo lilisababisha vifo vya watu 39 kwenye klabu ya usiku ya Reina.

Picha za muuaji huyo zilisambazwa na polisi baada ya kufanya shambulizi hilo
Amekamatwa katika mtaa wa Esenyurt mjini Istanbul.

Raia wa Israel, Ufaransa, Tunisia, Lebanon, India, Ubelgiji, Jordan na Saudi Arabia walikuwa miongoni mwa waliouawa huku mamia ya watu wakijeruhiwa.

ZeroDegree.
Aliyetekeleza shambulizi lililoua watu 39 Istanbul akamatwa Aliyetekeleza shambulizi lililoua watu 39 Istanbul akamatwa Reviewed by Zero Degree on 1/17/2017 10:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.