Loading...

39 wauawa kwa kupigwa risasi wakati wakiukaribisha mwaka mpya nchini Uturuki.

Mshambuliaji aliyetekeleza mashambulio hayo alitoroka na hajakamatwa hadi kufikia sasa.
Takriban watu 39 wakiwemo wageni 15 wanahofiwa kuuawa katika shambulio la klabu ya burudani mjini Istanbul Uturuki, kulingana na waziri wa maswala ya ndani nchini humo.

Mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakijiburudisha katika mgahawa huo wa Reina saa saba usiku wakati ambapo watu walikuwa wakisherehekea kuingia kwa mwaka mpya.

Waziri Süleyman Soylu ameelezea 
kuwa waliojeruhiwa ni 69. 

Kulingana na waziri wa maswala ya ndani takriban watu 39 wamefariki huku 69 wakijeruhiwa.

Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde kuanza kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo.

Baadhi yao iliwabidi kujirusha baharini kuepuka msusuru wa risasi zilizokuwa zinafyatulia.

Polisi mmoja ni miongoni mwa waliofariki.

Huku waliojeruhiwa wakikimbizwa hospitali, maafisa wa usalama wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo lakini muhusika wa shambilo hilo hajakamatwa bado.

ZeroDegree.
39 wauawa kwa kupigwa risasi wakati wakiukaribisha mwaka mpya nchini Uturuki. 39 wauawa kwa kupigwa risasi wakati wakiukaribisha mwaka mpya nchini Uturuki. Reviewed by Zero Degree on 1/01/2017 01:29:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.