Juma Kaseja ‘aizamisha’ Kagera Sugar.
Lawama zote zitamwangukia kipa wa Kagera Sugar, Juma Kaseja kwa kushindwa kukamata shuti la Razak Khalfan katika dakika ya 85 na mpira kujaa wavuni na kufanya Mwadui kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Ilipofika dakika ya 84, kila shabiki aliyekuwa uwanjani na waliokuwa wakitazama mpira huo, walijua kuwa utamalizika kwa sare ya 1-1.
Unajua ilikuwaje, ilifanyika madhambi umbali wa kama mita 40 kutoka katika lango la Kagera, mwamuzi akaamuru mpira wa adhabu.
Kagera walijipanga kuzuia mpira huo na Kaseja mwenyewe aliwapanga vizuri mabeki wake na wachezaji wengine.
Sasa, Razak akapiga shuti lile, lililofika mikononi mwa Kaseja, inawezekana aliudharau mpira ukamtoka ukawa unadundadunda upande wake wa kushoto.
Kaseja akauchumpia, kuurudisha, lakini ulikuwa umeshavuka mstari, na wakati anajaribu kuutoa, ukagonga posti na kuingia lakini akaurudisha.
Wakati anahangaika chini na mpira, wachezaji wa Mwadui hawakutaka kuhangaika naye zaidi ya kushangilia na kurudi katikati ya uwanja ndipo mwamuzi akaamuru mpira kuwekwa kati.
Kagera ndio walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Japhet Makarani dakika ya 38 kabla ya Mwadui kusawazisha dakika 48 kupitia kwa Awadhi Juma.

ZeroDegree.
Juma Kaseja ‘aizamisha’ Kagera Sugar.
Reviewed by Zero Degree
on
1/01/2017 01:34:00 PM
Rating: