Loading...

Ngoma awekwa chini ya uangalizi wa Madaktari Bingwa

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Yanga, Donald Ngoma, amekabidhiwa jopo la madaktari bingwa wa mifupa kuweza kumtibu tatizo lake la goti linalomkabili.

Akizungumza na waandishi wa habari, Daktari wa Yanga, Edward Bavu, alisema Ngoma anatarajiwa kurudi tena hospitali leo kwa ajili ya uchunguzi wa goti lake utakaofanywa na madaktari wawili baada ya kumaliza matibabu ya wiki mbili za mwanzo.

“Unajua Ngoma ni mgonjwa wa goti na kwa ukubwa wa tatizo lake, asingeweza kucheza ile mechi na Simba kwa hiyo mimi kwa kushirikiana na madaktari wenzangu, leo tutamwangalia tena ili kujua kama ataweza kukaa nje kwa muda gani,” alisema Bavu.

Katika hatua nyingine imeelezwa kuwa vitisho vya makomandoo, manyanyaso na kuwasemea umbea kwa viongozi, kumewafanya nyota wa Yanga kukosa morali, hamasa ya kucheza na kujituma na kusababisha timu hiyo kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Visiwani Unguja.

Chanzo cha ndani kutoka Yanga kilisema kuwa wachezaji wa timu hiyo wamekuwa wakiishi maisha ya mashaka na kutishiwa kupigwa na baadhi ya makomandoo, hasa pale inapotokea timu imefungwa au kutoka sare.

“Tatizo viongozi wanapenda watu wambea wambea ndio wamewaweka karibu, ukifanya kazi kwa kufuata misingi, makomandoo wanakuundia zengwe, sasa hivi wachezaji hawana morali sababu makomandoo wanawasakama sana, wanapeleka majungu kwa viongozi,” kilisema chanzo hicho.

“Sasa hivi kuna zengwe linasukwa eti wanadai daktari hafai kutokana na kila siku anasema uongo, eti Ngoma na Chirwa ni wagonjwa wakati si kweli, kwa hiyo kuna mipango ya kuhakikisha anapigwa chini na si yeye tu pia viongozi wengine wa juu wanadaiwa kuwa na damu ya upande wa pili,” kilisena chanzo hicho.

Source: Bingwa
ZeroDegree.
Ngoma awekwa chini ya uangalizi wa Madaktari Bingwa Ngoma awekwa chini ya uangalizi wa Madaktari Bingwa Reviewed by Zero Degree on 1/15/2017 11:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.