Loading...

Ferguson amtoa hofu Jose Mourinho

Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema kocha wa sasa wa Man United, Jose Mourinho hapaswi kuwa na hofu na matokeo ambayo wanayapata sasa kwani tayari ameshafanya kazi nzuri.

Ferguson amesema Van Gaal alifanya kazi nzuri lakini Mourinho amefanya kazi nzuri zaidi kwani kwa michezo 17 mfululizo hajapoteza mchezo hata mmoja na kinachohitajika sasa ni kuboresha kikosi chake ili kipate matokeo ya ushindi na kupambana na timu zilizo juu yake ili imalize ligi ikiwa katika nafasi za juu.

“Nadhani ameshafanya vizuri. Ni kama mchezaji mpya Manchester United, sio rahisi kuja na kubadili klabu kutoka kwangu, sio rahisi, nadhani Louis Van Gaal alifanya kazi nzuri na Jose amefanya kazi nzuri zaidi,

“Nafikiri bila kupata sare nyingi wangekuwa wanapambana na Chelsea, hiyo ni bahati mbaya, nafikiri anatakiwa aishi katika hali hiyo lakini mabadiliko yakiwepo kwenye timu,” alisema Ferguson wakati akifanya mahoajiano na BCC Sport.

ZeroDegree.
Ferguson amtoa hofu Jose Mourinho Ferguson amtoa hofu Jose Mourinho Reviewed by Zero Degree on 1/25/2017 11:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.