Loading...

FIFA yapitisha ongezeko la timu kombe la dunia, ,,hivi ndivyo jinsi mfumo wa timu 48 utakavyokua

Baada ya Baraza la FIFA kupiga kura kwa kauli moja na kupitisha ongezeko la timu zitakazoshiriki kombe la dunia hadi kufikia timu 48 kuanzia mwaka 2026 na kuendelea kuna maswali mengi yamejitokeza juu ya jinsi mfumo huo utakavo fanya kazi.

Haya ni majibu machache kwa maswali hayo, kama tunavyojaribu kufafanua mabadiliko yatakayofanyika.

Fuatilia hapa chini:

  • Kuongezeka idadi ya washiriki kutoka timu 32 hadi 48 katika Kombe la Dunia 2026.
  • Idadi ya michezo kwa ujumla itaongezeka kjutoka 64 hadi 80
  • Makundi yatakuwa 16 yenye timu tatu kila katika kila kundi.
  • Kila timu itacheza mara mbili katika hatua ya makundi
  • Kama mchezo wa kufuzu hatua ya makundi utaishia sare, matuta yataamua nani atakuwa mshindi.
  • Timu mbili zitakazoongoza kundi zitaenda kwenye Duru ya 32 bora.
  • Duru ya 32 bora itakuwa ni mtoano wa moja kwa moja, na kisha Duru ya 16, kisha robo fainali, nusu fainali, na mwisho fainali.
  • Timu itacheza hadi mechi 7 tu kama itafika fainali, ambayo ni idadi sawa na mfumo wa timu 32.
  • Mashindano hayo ya kombe la Dunia yatadumu kwa siku 32, ikiwa ni sawa na muda uliotumika katika Kombe la Dunia mwaka 2014.
  • Timu nne za ziada kutoka shirikisho la soka la Asia na Afrika zitaongezeka, wakati timu tatu zaidi kutoka Ulaya pia ubora zitaongezeka.
  • CONCACAF inapata uwezekano wa ongezeko kutoka timu 3.5 hadi 6.5 (.5 ikiashiria mchujo) pamoja timu nyingine 6 kati ya timu 10 kutoka ukanda wa CONMEBOL(Amerika) watafuzu.
ZeroDegree.
FIFA yapitisha ongezeko la timu kombe la dunia, ,,hivi ndivyo jinsi mfumo wa timu 48 utakavyokua FIFA yapitisha ongezeko la timu kombe la dunia, ,,hivi ndivyo jinsi mfumo wa timu 48 utakavyokua Reviewed by Zero Degree on 1/11/2017 01:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.