Loading...

Hatimaye 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi mgodini Geita waokolewa

Wachimbaji madini 15 wameokolewa wakiwa hai baada ya mgodi wao kupolomoka siku tatu zilizopita.

Ajili hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita, tarehe 26 Januari, katika mgodi uitwao RZ Gold Mine, unaomilikiwa na raia wa China katika machimbo ya dhahabu yaliyopo Geita Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Manusura hao ni raia 14 wa Tanzania na mmoja wa China.

Mwandishi wa BBC Halima Nyanza aliyeshuhudia zoezi la uokoaji anasema eneo hilo lilijawa na shangwe na vilio vya furaha wakati ndugu, jamaa na wachimbaji wengine walipokuwa wakishuhudia uokoaji wa manusura hao.



Manusura hao walionokena wadhaifu kiafya, lakini walipatiwa huduma ya kwanza mara moja na kisha kupelekwa katika kituo cha afya kilichopo jirani

Uchunguzi wa nini hasa kilisababisha ajali hiyo unaendelea, lakini hii si mara ya kwanza kwa tukio kama hili kutokea

Mwaka jana mwezi Novemba, Tanzania ilisherehekea ukoaji wa 'kimiujiza' baada ya wachimbaji watano kuokelewa wakiwa hai baada ya kukwama chini ya ardhi kwa siku 41.

Eneo la Magharibi mwa Tanzania lina migodi mingi na wachimbaji wengi hutoka vijiji vya jirani.



Hata hivyo migodi mingi haikaguliwi mara kwa mara na hali ya usalama ya migodi hii haitimizi viwango rasmi.

Naibu waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani, amesema serikali itahakikisha wachimbaji wana kuwa salama.

Mgodi huo utakuwa chini ya uangalizi kwa siku tano kabla wachimbaji kuruhusiwa kufanya kazi.

Naibu waziri pia amewaagiza makamishina wa madini kufanyia tathmini migodi mwingine ya wachimbaji wadogo kwa siku tano, kuanzia kesho



Source: BBC Swahili
ZeroDegree.
Hatimaye 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi mgodini Geita waokolewa Hatimaye 15 waliokuwa wamefukiwa na kifusi mgodini Geita waokolewa Reviewed by Zero Degree on 1/29/2017 06:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.