Waokoaji mgodini Geita wapokea ujumbe toka kwa waliofukiwa na kifusi
- Hali bado ni tete kazi ya uokoaji waliofukiwa mgodini Geita
- Watu 14 wafukiwa na kifusi cha udongo mgodini
Jana, watu hao walituma ujumbe uliotaja majina yao na idadi kwamba wako 15, tofauti na 14 kama ilivyokuwa ikiripotiwa awali.
Taarifa kutoka mgodini zilizolifikia gazeti hili zilieleza kuwa, baada wachimbaji hao kugundulika kwa mara ya kwanza walipofikiwa na bomba, walirudisha ujumbe kueleza idadi yao na kwamba walikuwa na njaa na kiu hivyo wakaomba watumiwe sigara, soda na maji.
Akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Nishati, Medadi Kalemani, mmoja wa watu waliopo katika timu ya uokoaji, Felix Adolf alisema licha ya maombi hayo, ilishauriwa kuwa watu hao waliofukiwa watumiwe maji ya glucose yanayochanganywa na timu ya madaktari iliyopo hapo.
Wachimbaji hao waliofukiwa na kifusi cha udongo kwa zaidi ya siku tatu sasa katika Mgodi wa RZ mkoani Geita, wamekuwa wakiwasiliana kwa kutumia bomba la kuchimbia maji.
Katibu wa wachimbaji wadogo katika Mkoa wa Geita, Golden Hainga alisema jana kuwa kazi ya kuchimba ili kuingiza bomba la kuwapelekea maji na chakula wachimbaji hao walioko chini, ilifanikiwa na waligonga bomba hilo kuashiria kuwa wako hai.
ZeroDegree.
Waokoaji mgodini Geita wapokea ujumbe toka kwa waliofukiwa na kifusi
Reviewed by Zero Degree
on
1/29/2017 10:56:00 AM
Rating: