Loading...

Ziara ya kwanza ya Rais Magufuli nje ya Afrika Mashariki [EAC]

Rais John Magufuli akisalimiana na Rais wa Mungano wa Visiwa vya Comoro, Azali Assoumani walipokutana kwenye ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam jana akiwa safarini kuelekea Addis Ababa, Ethiopia kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa 28 wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika (AU). Rais Assoumani alikuwa akitokea Comoro kupitia Dar es Salaam. (Picha na Ikulu).
RAIS John Magufuli ameondoka nchini na kuelekea Addis Ababa, Ethiopia ambako atahudhuria Mkutano Kilele wa 28 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) unaoendelea nchini humo.

Ziara hiyo ni ya kwanza kwa Rais Magufuli kutoka nje ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) tangu aingie madarakani kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Novemba 5, mwaka jana.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu Dar es Salaam jana ilisema katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wa jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli aliagwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Wengine waliojumuika kumuaga Rais Magufuli ni viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda.

Kwa mujibu wa Ikulu ya Dar es Salaam, pamoja na kuhudhuria mkutano huo, akiwa Addis Ababa, Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Bara la Afrika wanaohudhuria mkutano huo.

Source: Habari Leo
ZeroDegree.
Ziara ya kwanza ya Rais Magufuli nje ya Afrika Mashariki [EAC] Ziara ya kwanza ya Rais Magufuli nje ya Afrika Mashariki [EAC] Reviewed by Zero Degree on 1/29/2017 10:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.