Loading...

Henry amshawishi Ozil kubaki Arsenal

Mchezaji wa zamani wa Arsenal ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka, Thierry Henry amemwomba Mesut Ozil kuacha mpango wake wa kutaka kuondoka Arsenal na kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya London kwa muda mrefu zaidi.

Henry amesema kuwa anafahamu fika matatizo ambayo yanamkabili kwa sasa Ozil kwani hata yeye yameshamfika lakini jambo ambalo Ozil analitaka anaweza kulifanikisha hata akiwa Arsenal lakini tu kama atakubali kusaini mkataba mpya.

“Nimekata tamaa kama anaweza kubaki, lakini naelewa tatizo, ni kama hali iliyonikuta mimi 2007 wakati najiunga Barcelona na moyo ukiwa mzito. Sijui mipango ya Arsene [Wenger] labda na yeye anamaliza mkataba wake,

“Mesut ameshinda Kombe la Dunia akiwa na Ujerumani. Lakini kwa klabu ana kombe moja tu akiwa na Real Madrid 2012. Atakuwa na matatizo sana, lakini anaweza kufanya hivyo akiwa Emirates ndiyo maana ninamuhimiza abakie Arsenal na kuja kuwa mtu mwenye historia na Arsenal,” alisema Henry.

ZeroDegree.
Henry amshawishi Ozil kubaki Arsenal Henry amshawishi Ozil kubaki Arsenal Reviewed by Zero Degree on 1/22/2017 07:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.