Loading...

Kikosi bora cha FIFA kwa mwaka 2016


Siku ya Jumatatu wakati wa utoaji wa tuzo za FIFA Zurich, nchini Uswisi, kikosi bora cha FIFA kwa mwaka wa 2016 kilitangazwa.

Kikosi bora cha wachezaji 11 duniani kimechaguliwa na wachezaji 26,516 katika taratibu za kitaalamu kote duniani ambao kura zao zilizopigwa ndizo zilipelekea kutajwa kwa kikosi hicho, kwa mara nyingine tena Barcelona na Real Madrid zikiongoza.

Cristiano Ronaldo, Sergio Ramos, Marcelo, Toni Kroos na Luka Modric wote walijumuishwa, kama ambavyo ilikuwa kwa Barcelona ambapo Gerard Pique, Andres Iniesta, Luis Suarez na Lionel Mess wakijumuishwa na Dani Alves ambaye alianzia Barcelona mwaka 2016 na kumalizia msimu akiwa Juventus. Mwakilishi wa pekee kutoka Bundesliga ni Goli kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer.

Orodha ifuatayo chini ni kikosi 
Bora kamili cha FIFA:

Kipa

  • Manuel Neuer
Mabeki
  • Dani Alves
  • Gerard Pique
  • Sergio Ramos
  • Marcelo
Viungo
  • Luka Modric
  • Toni Kroos
  • Andres Iniesta
Washambuliaji
  • Lionel Messi
  • Luis Suarez
  • Cristiano Ronaldo
Kikosi bora cha FIFA kwa mwaka 2016 Kikosi bora cha FIFA kwa mwaka 2016 Reviewed by Zero Degree on 1/09/2017 11:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.