Loading...

Ronaldo amgaragaza Messi, ..ashinda tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa mwaka 2016

Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa mchezaji bora katika sayari hii kwa mara ya nne sasa akiwa katika kazi yake ya soka.

Katika tuzo mpya za FIFA zilizozinduliwa, Ronaldo mwenye umri wa miaka 31, ndiye mshindi wa tuzo hizo akiwapita nyota kama Lionel Messi wa  Barcelona na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid.

Akizungumza nchini Zurich, Uswisi siku ya leo Jumatatu, nyota huyo wa Real Madrid alikuwa na furaha sana na kusema haya.



"Kama nilivyoeleza kwa mara nyingi, mwaka jana ulikuwa mwaka wa ndoto na matukio ya ajabu kwangu," Ronaldo alisema. "Nikiwaa na Real Madrid tumepata kushinda Ligi ya Mabingwa, nikiwa na timu ya taifa tulipata kushinda kikombe cha Ulaya kwa mara ya kwanza katika historia. Siwezi kuamini kabisa matukio haya yaliyotokea kwa mwaka jana. Hivyo ni fahari na furaha kwangu. Inanipasa kusema asante kwa wachezaji wenzangu wa Real Madrid na wale wa timu ya taifa na makocha pia. Kweli ni mwaka wa ajabu kwangu. "

Awali 
Ronaldo alishinda tuzo hii mwaka 2008, 2013 na 2014 ikiwa ni kama ushindani kati yake na Messi ambaye kwa sasa anaongoza kwa kupata tuzo hiyo mara nyingi kwa muongo mmoja uliopita.

Tuzo hiyo ilitolewa katika hafla iliyofanyika leo kama vile imevyoweza kuonekana wakati ambapo FIFA ilianza utaratibu wake wa kutoa tuzo zake binafsi baada ya ushirikiano wa muda katika tuzo za Ballon d'Or nchi ya Ufaransa kati ya 2010-15 ambayo zamani ilikuwa ndiyo taji kwa mchezaji bora wa mwaka.

Ronaldo pia alishinda tuzo ya Ballon d'Or katika mwaka wa 2016 na si vigumu kuelewa ni kwanini tuzo hiyo alipewa yeye.

Nyota huyo wa Ureno alifunga mabao 51 ndani ya michezo 48 katika mashindano yote, na kuwaongoza Real Madrid katika msimu wa 2015-16 kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya wapinzani wao Atletico Madrid. 

Ronaldo huyo huyo pia alikuwa na mchango mkubwa kwa taifa lake la Ureno kushinda ubingwa wa Euro 2016 alipokuwa nahodha wa taifa lake kwa kulipa ubingwa taifa lake kwa mara ya kwanza katika historia.

Ushindi wa tuzo hiyo umempa heshima kubwa Christiano Ronaldo na kumweka miongoni mwa mashujaa wakubwa katika mchezo wa soka bila shaka yoyote, na hii tuzo ni ya mwisho katika kuufunga mwaka wa 2016 ikiwa vizuri kwake na kumfanya anayestahili kuendelea katika jitihada binafsi za kupambana na Messi.

Katika suala la tuzo za Mchezaji bora 
Duniani  sasa rekodi ya ushindi wa tuzo hiyo inasoma kama ifuatavyo: Messi 5-4 Ronaldo.

ZeroDegree.
Ronaldo amgaragaza Messi, ..ashinda tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa mwaka 2016 Ronaldo amgaragaza Messi, ..ashinda tuzo ya FIFA ya mchezaji bora wa mwaka 2016 Reviewed by Zero Degree on 1/09/2017 11:57:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.