Loading...

Jengo la ghorofa 17 laporomoka Iran na kuua watu 75 wakiwemo waokoaji 45 [Picha]

Wazima moto wengi wanahofiwa kuaga dunia baada ya jengo moja kubwa kwenye mji mkuu wa Iran Tehran, kushika moto na kuporomoka.

Wazima moto 200 walikabiliana na moto huo kwenye jengo hilo la ghorofa 17 kwa saa kadha, kabla ya kuporomoka kwa sekunde chache.

Jengo hilo ambalo ujenzi wake ulikamilika mwaka 1962, lilikuwa wakati mmoja jengo refu zaidi mjini Tehran.

Moto huo unaripotiwa kuanza mwendo wa saa 04:30 GMT siku ya Alhamisi, wakati watu hawakuwa bado wameingia.



Wazima moto walikuwa wamepambana na moto huo kwa saa kadha

Magari kumi ya kuzima moto yalifika eneo hilo na vituo vya runinga viliripoti kuwa wazima moto kadha walikuwa ndani ya jengo wakati liliporomoka.

Kituo kimoja cha runinga cha serikali kilinukuu afisa mmoja akisema kuwa kati ya watu 50 na 100 wanaaminiwa kukwama chini ya vifusi.




ZeroDegree.
Jengo la ghorofa 17 laporomoka Iran na kuua watu 75 wakiwemo waokoaji 45 [Picha] Jengo la ghorofa 17 laporomoka Iran na kuua watu 75 wakiwemo waokoaji 45 [Picha] Reviewed by Zero Degree on 1/20/2017 10:16:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.