Loading...

Jina na nembo mpya ya Benki ya Posta Tanzania vyazinduliwa na Waziri Mpango

Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango Januari 19, 2017 amezindua jina jipya na nembo mpya ya Benki ya Posta Tanzania (TPB) ambayo itatumika kwa jina la TPB Bank Plc.

Akizungumza baada ya kuzindua jina na nembo mpya, Dkt. Mpango amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano ili benki hiyo ijiimarishe kimtaji na kutekeleza majukumu yake.

“Nimefarijika kusikia kuwa benki hii imefanikiwa kupeleka huduma zake za kibenki pembezoni mwa nchi, kujenga na kufungua matawi kwenye miji mikuu yote nchini,” amesema.

Dkt. Mpango ameiagiza Bodi ya Wakurugenzi ya TPB Bank Plc kuhakikisha inapeleka gawiwo la serikali kwa wakati.

“Benki yenu ihakikishe inaishawishi serikali kuendelea kuwekeza kwa kuipa gawiwo lake la faida kwa wakati na inavyostahili,”

Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB Bank, Sabasaba Moshingi amesema lengo la kubadilisha jina na nembo ni kwenda sambamba na mabadiliko ya kuiboresha benki.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPB, Prof. Lettice Rutashobya alimhakikishia Dkt. Mpango kuwa benki hiyo itaendelea kutoa huduma bora kwa wateja ikiwa ni pamoja na kuwafikia watanzania wengi hasa walioko pembezoni ili waweze kunufaika na huduma za kibenki zinazotolewa na benki hiyo.

ZeroDegree.
Jina na nembo mpya ya Benki ya Posta Tanzania vyazinduliwa na Waziri Mpango Jina na nembo mpya ya Benki ya Posta Tanzania vyazinduliwa na Waziri Mpango Reviewed by Zero Degree on 1/20/2017 11:41:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.