Loading...

Maofisa wote wa ngazi za juu waliofanya kazi kipindi cha Obama wajiuzulu serikalini

Maofisa wote wa ngazi za juu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani waliofanya kazi kipindi cha uongozi wa Rais mstaafu, Barack Obama wamejiuzulu.

Gazeti la Washington Post limeandika kuwa, kujiuzulu kwa wakurugenzi na maofisa wote wa ngazi za juu ni sehemu ya mwenendo wa kuachia ngazi maofisa wa ngazi za juu wa Serikali iliyopita ambao hawataki kufanya kazi na Rais Donald Trump.

Kujiuzulu kwa pamoja maofisa wote wa Wizara ya Mambo ya Nje kunatatiza kazi ya Rais Trump katika sekta ya masuala ya kigeni.

Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Patrick Kennedy ambaye amekuwa na nafasi kubwa katika mchakato wa kuhamisha madaraka na ilidhaniwa kuwa, pengine angeendelea kufanya kazi katika kipindi cha uongozi wa Trump, naye alijizulu Jumatano iliyopita katika hatua iliyowashangaza wachambuzi wengi wa masuala ya Marekani.

Wakurugenzi wengine wakuu waliojiuzulu nyadhifa zao katika wizara hiyo ni Gregory Starr, Michele Bond na Tom Countryman.

Hivi karibuni, Rais Trump alitangaza kusimamisha ajira za mabalozi wote duniani.

Katika hatua nyingine, mamia ya wakazi wa Jiji la New York wamemiminika barabarani ikiwa ni kuonyesha kupinga misimamo Rais Trump.

ZeroDegree.
Maofisa wote wa ngazi za juu waliofanya kazi kipindi cha Obama wajiuzulu serikalini Maofisa wote wa ngazi za juu waliofanya kazi kipindi cha Obama wajiuzulu serikalini Reviewed by Zero Degree on 1/28/2017 09:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.